Tuesday, 12 July 2016

KWELI UKIWA KADA WA CCM TAALUMA YAKO LAZIMA UIEKE PEMBENI.



SALIM KIKEKE naye kaingia katika kundi la akina Pole Pole ambao wote walipendwa katika nyakati tofauti na kuaminiwa kua ni wasomi wanaojielewa lakini baada ya kuonyesha ukada wao kwa vitendo wamepoteza sifa za taaluma zao na kuchukiwa na mashabiki zao. Mimi ndio maana naogopa kua CCM maana naamini itanilazim kuitia kapuni elimu yangu na kufata ujinga wa watu wachache.

Inashangaza mtu kama Salim Kikeke anaetoa taarifa mbali mbali diniani zenye kusisimua na kuwafunza walimwengu mambo mbali mbali yanayoikabili dunia hasa yale ya unyanyasaji, ukandamizaji na kutofata sheria na misingi ya demokrasia na utawala bora kuona leo anakubali utata wa Jecha Salim Jecha lakini anamuuliza Maalim kwa nini alisusa kwenda kupiga kura na kudai eti Maalim kawakosesha wafuasi wake haki yao ya msingi.

Ivi ni haki gani anayoikusudia Salim Kikeke ambayo kupitia uchaguzi wa marejeo Wazanzibari wangeipata? Wazanzibari kwetu sio haki kupata wawakilishi bali haki yetu ni kumpata raisi wetu Maalim Seif ili atuongoze kuelekea Singapore.  Je Salim Kikeke anamaanisha kua kama Maalim angeshiriki uchaguzi huo wa marejeo haki hiyo ingepatikana? Na kwanini kama ingepatikana haikupatikana tarehe 25 October ambapo Wazanzibari wengi tulimchagua Maalim Seif kua rais wetu?

Salim Kikeke kaishusha hadhi kazi yake na taaluma yake na inawezekana kumbe yale anayoyatangaza kila siku hayamfunzi chochote katika maisha yake ya kila siku.

Salim Kikeke kawadhalilisha na kuwatoa thamani Watanzania kutokana na kutetea batil ambayo hakuna hata mmoja asiejua kua ni batil.

Naamini hata hao waliomuajiri sasa wataanza kumfkiria upya na kumchukulia hatua kwa kushabikia mambo ambayo waliomuajiri wanatumia mda wao mwingi kuyapiga vita duniani kote (ukandamizwaji wa demokrasia).

Salim Kikeke hata akipayuka vipi hawezi kuisaidia CCM katika hili wala hawezi kuipotosha dunia ikaamini kua chama chake kilitenda haki wakati kila mtu duniani anajua kua kimetenda batil.

Nadhani Salim Kikeke angejifunza kwa Mu Africa mwenzake Shaka ambaye alitumia taaluma yake vizuri na kuuliza maswali ya msingi kwa ustaarabu wa hali ya juu tena kwa lugha ya ki- ingereza lakini kila mtu alielewa mjadala wake.

Salim Kikeke aliuharibu mjadala ule makusudi akijua kua watu wengi duniani wanafatilia na kukipenda sana kipindi chake ndio maana akaamua kuuharibu kwa lengo la kuificha dunia isijue kile kilichotokea Zanzibar na yale yanayoendelea Zanzibar ambayo yanafanywa na chama chake akidhani labda itasaidia ila kwa hakika Salim Kikeke kachelewa sana kukisaidia chama chake na kwa bahati mbaya Salim Kikeke kafunga banda wakati kuku washatoka.


No comments: