*"UGAIDI WA MASHEIKH MIAKA YOTE USHAHIDI HAKUNA, LAKINI "UGAIDI WA MBOWE USHAHIDI TAYARI NA KESI CHAPUCHAPU KULIKONI?*
*Masheikh waachiwe huru polisi ikipata ushahidi iwalete mahakamini*
*MAONI YA Sauti ya wazalendo halisi Africa*
Kwa mara ya kwanza mtuhumiwa wa kesi ya ugaidi asiyekua Muslimu apatikana Tanzania.
Mh Freeman Mbowe mwenyekiti wa chama cha upinzani Chadema amekabiliwa na tuhuma za ugaidi.
Dunia imemshuhudia kamanda wa jeshi la Polisi Mh IGP Simoni Siro mbele ya vyombo vya habari akitamba kuwa: "Jeshi la Polisi lina ushahidi wa kutosha na ushahidi umekamilka Kwa tuhuma za Mh Mbowe."'
Dunia inataka kuaminishwa vijana watatu waliokuwa walinzi wa Mheshimiwa Mbowe amabo wote ni waislamu kuwa Waislam uwa Tanzania wanahusishwa na ugaidi hili kwa Waislamu wa Tanzania wanatakiwa wafikiri zaidi nini kitakachoendela kupikwa na utawla wa CCM dhidi ya Waislamu
_Dunia imepata mshangao mkubwa sana kumbe jeshi la polisi linaweza Kupata ushahidi wa tuhuma za ugaidi kwa haraka hivo na kesi kuanza kwenda chapuchapu kiasi hicho mpaka kwa njia ya mtandao? ????.?_
Kwanini jeshi la polisi limekosa ushahidi wa tuhuma za ugaidi kwa Masheikh, Maimamu na Waalimu wa Madrasa Zaid ya 200. waliojazwa mahabusu mbalimbali za Tanzania kwa zaidi ya miaka Mitano kwa madai upelelezi haujakamilika na hata mahakamini hawapelekwi tena kwa muda mrefu na hakuna uhakika kama upelelezi huo unaendelea!!.
Wazalenzo halisi Africa tunakuomba Mh Kamanda Siro ujitokeze tena mbele ya dunia kupitia vyombo vya habari uieleze dunia Kwanini uliwakamata masheikh ili Hali hauna ushahidi wa makosa yao? ??
Njoo Kamanda Siro uieleze Dunia Kwanini umeshindwa kuthitibisha tuhuma za ugaidi kwa Masheikh kwa miaka Mitano na Zaidi na bado unaendelea kuwashikilia? ??
*Je waislamu wakisema imetungwa sheria ya ugaidi kupambana na uislamu Watakuwa wamekosea? ????*
Waislamu wakisema jeshi la polisi linatumia vibaya sheria ya ugaidi kupambana na waislamu je watakua wamekosea? ?????
Ikiwa leo masheikh Zaidi ya 200 kwa miaka Zaidi ya mitano mumewapa tuhuma za ugaidi lakini hadi sasa hakuna ushahidi je huku sio kutumia kivuli cha ugaidi kuwakomoa waislamu? ??
Wazalenzo halisi Africa hatujasahau mauaji ya imamu aliyekuwa mwanafunzi wa chuo kikuu alipouawa kwa kupigwa risasi akipita bank wilayani Temeke eneo la mtoni na kesho yake Mh Siro uliitangazia dunia kuwa imamu Salumu alikua gaidi kwasababu alisikika akisema "Allah akbar"
Haukupita muda Mh Siro ukapanda cheo kuwa IGP kutoka kuwa RPC wa mkoa wa Dsm, bado kuna maswali mengi sana kifo cha Imamu Salumu na Tamko la kamanda Siro ndiyo limempandisha cheo au kitu gani? ???
Na je ilifaa kweli kumpandisha cheo mara baada ya kuwajeruhi waislamu waliokua Wana uchungu wa mwenzao kuuawa na Kamanda Siro kuhalalisha kifo cha imamu Salumu kwakusema Allah akbar? ???????
Wazalendo halisi wanatoa wito kwa jeshi la polisi kujitokeza Tena hadharani kuitangazia dunia kuwa haijapata ushahidi wa tuhuma za ugaidi za masheikh na hivo waachiwe huru.
Wazalenzo halisi wanalipongeza jeshi la polisi kufanya uchunguzi haraka kwa tuhuma za Mh Mbowe na kuipeleka kesi haraka Haraka mpaka kwa njia ya mtandao ili imalizike haraka
Lakin wazalendo halisi wanahoji kwanini jeshi la polisi limeshindwa kufanya haraka hiyo kwa masheikh wenye tuhuma kama za Mh Mbowe? ????
Wazalendo halisi wanahoji au kwakuwa wale masheikh ni waislamu?
Washatkiwa,, watatu wanaoshtakiwa na Mbowe wote ni Waislamu isipokuwa Mbowe itabidi kwa hili tumbadili jina mheshiwa Mbowe tumuite, Mheshimiwa Hamisi Mbowe kuonesha jinsi ugaidi unavyosingiziwa kwa Waislamu wa Tanzania.
Imekuaje uchunguzi wa Mheshimiwa Hamisi Mbowe umekamilika kama miujiza?
Waislamu wa Tanzania kwa hili la ugaidi wanatakiwa wafikiri kwa mapana.
Au kwakuwa mataifa ya nje ikiwemo Marekani wameanza kuinyoshea kidole nchi yetu ?
Je jeshi la polisi linataka waislamu pia waanze maandamano yasiyoisha kushinikiza kuachiwa masheikh ndiyo kesi itaenda na ushahidi utakuwa tayari? ?
Pia kulikoni waislamu wamegawanywa kwa mafungu baina ya Waislamu wa bara na wa Zanzibar wale masheikh wa Zanzibar wameonekana hawana hatia hawa wa huku kwetu wanaozea magerazani?
*#WAACHIWE MASHEIKH, AACHIWE MH MBOWE WAWE HURU WOTE SIO MAGAIDI#*
*Sauti ya wazalendo halisi*
No comments:
Post a Comment