Tuesday 31 December 2013

KIKWETE KUIPIGANIA HOJA YA MTIKILA YA TANGANYIKA ? AU MTEGO WA KATIBA KUBAKI ILE ILE

Kura hii ya maoni kuinusuru CCM Na Fedheha pande zote mbili za Muungano za CCM wakatae serkali mbili Wakubali matakwa ya wananchi walio wengi.
Hii ndio magic number ya 2015 CCM watch out !
Tanganyika 

Waliotaka serkali tatu CUF /Chadema?NCCR Mageuzi, Tanganyika  61% 
Waliotaka serkali mbili CCM   Tanganyika 24 %
Walioataka serkali moja 13%

Zanzibar
Walioataka Muungano wa Mkataba kwa Zanzibar 60%
Walioataka serkali mbili CCM upande wa  Zanzibar  34% 
0.1% Walitaka serkali moja 
Kwa Wale waliopata kuipitia Rasimu mpya ya katiba wanasema Watanganyika wamepewa upendeleo na Wazanzibari hoja zao zimetiwa Kapuni. Watanganyika , kupata Bendera yao , Katiba yao kupata nafasi 50 hamsini kwenye Bunge La Muungano wakati wa Wazanzibari kupata nafasi 20. Hoja kubwa ya wazanzibari asilia 60% walioataka muungano wa Mkataba imekataliwa na imekubaliwa ya wale asilimia ndogo ya 34 % ya CCM . Hoja ya Wazanzibari kuwa wamechoka Mabomu ya Machozi wanahitaji jeshi la Polisi lenye kuheshimu haki za binadamu ili Waunde Jeshi lao pia rasimu ya kwanza ilikubali ila  rasimu ya pili imetoa na kufanya jeshi moja tu la Polisi.“Rasimu inapendekeza kuwepo na Jeshi moja la polisi na Idara moja ya Usalama kwa taifa zima, siyo kama tulivyokuwa imependekezwa katika rasimu ya kwanza kwamba kila upande unaweza kuanzisha jeshi lake la polisi.Hapa sasa Serikali ya Tanganyika na ya Zanzibar zitabaki na nini kama Usalama na Polisi utakuwa chini ya Muungano? zitakua serikali lege lege zisizo na nguvu ya kusimamia serikali zake  zitakua serkali zilizokosa Mwega .Kwangu mimi sioni tatizo liko wapi kwa Tnaganyika na Zanzibar kuwa na jeshi lake  kuweza kuwa na uwezo wa kutimiza ahadi zao ikiwemo ilani za vyama tofauti ni kupinga vita rushwa na kupunguza uhalifu suali la jee ikiwa Rais wa Muungano ni wa Chama chengine na Zanzibar ni Chama chengine si kutakua na kuhujumiana !Ni Makosa makubwa kwa Tanganyika na Zanzibar kukosa kuwa na Jeshi lake la Polisi.

Hii ni Bendera ya Tanganyika iliotumika kuanzia mwaka 1961 hadi mwaka 1964.
Walioshinda ni Kina Mtikila kutaka hoja yake yakugombea bila Chama imepita kwenye rasimu ya pili.
Wanadiaspora wameekewa Mtego hakuna uwazi kama katiba ya Kenya inayosema wazi Kweney katiba yao kuwa Wakeny, Waganda ,a WaRwanda wa anaweza kuwa na uraia zaidi ya mmoja very simple bila kupaka mafuta nyuma ya chupa kama rasim uya ktiba ilivyojipaka mafuta nyuma ya chupa !
Rais Jakaya Kikwete amewataka wajumbe watakaopata fursa ya kuingia kwenye Bunge la Katiba kuweka mbele masilahi ya Taifa badala ya makundi yao.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa Ripoti na Rasimu ya Pili ya Mabadiliko ya Katiba jana, Rais Kikwete alisema kuingiza hulka binafsi katika mchakato huo ni kuchelewesha upatikanaji wa Katiba Mpya kwa muda uliopangwa.
Alisema alipofanya mazungumzo na vyama vya siasa vya Chadema, NCCR-Mageuzi, TLP na CUF, aliwataka kuweka kando masilahi ya vyama vyao na kutanguliza utaifa ili kupata Katiba yenye sura ya taifa.
“Niliwaambia na leo (jana) narudia kuwa watakapokuwa wakiijadili rasimu, watambue kuweka mbele masilahi ya taifa, malengo ya vyama na asasi zao yawe ya pili. Kama hawatafanya hivyo hatutapata Katiba,” alisema na kuongeza:
“Kama itashindikana kupata Katiba Mpya, hakutakuwa na katiba ya mpito… hii tuliyonayo sasa itaendelea kutumika, nawaelezeni na ikihitajika tena mchakato utatakiwa kuanza mwanzo na mimi nitakuwa nimesshastaafu nipo kijijini Msoga (Chalinze, Pwani).”
Alisema Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba walitoka maeneo tofauti hivyo kutofautiana malengo, lakini kutokana na uzito wa uundwaji wa Katiba, waliweka kando tofauti zao na ndiyo maana rasimu waliyoiandaa ina sura ya kitaifa.
“Wajumbe wanatakiwa kuiga mfano wa Wajumbe wa Tume ambao waliweka kando tofauti zao na leo hii wamekuja na rasimu iliyo na sura ya kitaifa. Nanyi mnatakiwa kufanya vivyo hivyo,” alisema na kuongeza:
“Mtambue pia kuwa hatima ya katiba iko mikononi mwa wananchi, hivyo msifanye mnavyojua, isomeni rasimu kuanzia sura ya kwanza hadi ya mwisho ili muweze kutoa maoni na mapendekezo kwa ufasaha zaidi kuliko kuchagua maeneo ya kuchangia.”
Rais Kikwete alisema kukamilika kwa rasimu hiyo kunatoa nafasi kwa mchakato wa kuwapata Wajumbe wa Bunge la Katiba ili ifikapo Februari 11, mwakani Bunge hilo liwe limeanza.

No comments: