Tuesday 21 January 2014

LIPUMBA AZINDUA KAMPENI ZA UWAKILISHI KIEMBESAMAKI

Uzinduzi wa Kampeni ya CUF Jimbo la Kiembesamaki na Kumtangaza Mgombea Wake.

Mgombea wa CUF akinadiwa katika mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Kiembe Samaki Abdulmalik zilizozinduliwa leo na.Mwenyekiti wa chama hicho Professor Lipumba
  




Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Professa Ibrahim Haruna Lipumba akimnadi mgombea wa Chama hicho katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki, Abdulmalik Haji Jecha, katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki zilizofanyika Bustani ya Kiembesamaki, Wilaya ya Magharibi Unguja
Mwenyekiti wa chama cha Wananchi CUF Taifa Profesa Ibrahim Haruna Lipumba amewataka wananchi wa Jimbo la Kiembesamaki kumchagua kiongozi atakayeweza kuingia katika bunge la katiba na kuyatetea na kuleta maslahi ya Zanzibar. Kauli hiyo ameitoa jana huko Kiembesamaki wakati alipokuwa akizindua kampeni na kumtambulisha mgombea uwakilishi kupitia chama hicho.
Amesema kiongozi bora ni yule atakaeweza kuitetea Zanzibar na kuipatia maendeleo na kupata mamlaka yake kamili pamoja na  kuleta mabadiliko. Aidha ameeleza kuwa CUF inataka kuleta mabadiliko katika mambo ya muungano na kuona kuwa haki inafanyika katika nchi zote.Aidha amesema kupita chama cha CUF wananchi watapata kiongozi mzuri atakaeweza kuingia kwenye bunge la katiba na kuitetea nchi bila ya woga wala kupoteza mwelekeo. “Mpeleke mtu atakaeweza kuingia kwenye bunge la katiba na kutetea maslahi ya Zanzibar”, alifahamisha.Hata hivyo amesisitiza kuwa uchaguzi ufuate utaratibu uwe huru na haki bila ya kushirikisha vyombo vyengine. 
Nae mgombea uwakilishi AbdulMalik Haji Jecha amesema pindipo wananchi watamchagua ataitetea Zanzibar kwa moyo wa uzalendo na kuleta maendeleo kwa maslahi ya nchi.Uchaguzi huo mdogo wa jimbo la Kiembesamaki unafanyika kutokana na aliyekuwa mwakilishi wa Jimbo hilo Mansour Yussuf Himid kuvuliwa uwanachama kupitia CCM.



Mheshimiwa Hamad Masoud  



No comments: