Thursday, 25 December 2014

TATHMINI YA JULIUS MTATIRO JUU YA HOTUBA YA RAIS KIKWETE

Julius S. Mtatiro· 
TATHMINI YANGU, HOTUBA YA RAIS KIKWETE - WIZI WA FEDHA ZA TEGETA ESCROW.
1. Nilitarajia angezungukazunguka ili kujaribu kuokoa mwizi huyu au yule - Imekuwa hivyo.
2. Kwa kiasi kikubwa maazimio ya bunge ameyakwepa kwepa tu, ilimradi asiyatekeleze kabisa au akitekeleza iwe hivyo nje ya wakati.
3. Rais ameshindwa kuongea kama mkuu wa nchi, kuwaonesha watendaji na washirika waje kuwa anachukia rushwa, haitaki na anaipiga vita. Kila aliyehusika na wizi wa fedha hizi au mgao wake, rais hasemi kwa uwazi kuwa amevunja taratibu za uongozi, anazungukazunguka.
4. Bodi ya TANESCO ilipaswa kufukuzwa kazi, si kuacha ati imalizie muda wake kwa sababu uko ukingoni. Mchezo huu ni kama ule wa EPA, badala ya kuwaadhibu wezi na kuwaondoa madarakani , wanaombwa warudishe fedha tu.
5. Rais anaonekana hajui msingi wa uchunguzi wa ripoti ya CAG na majumuisho ya PAC. Au amepotosha kila kitu kimakusudi, anahitaji uchunguzi mpya kuchunguza nini ambacho vyombo vya serikali na bunge havijachunguza?
6. Inaonesha wazi kuwa, rais hayuko tayari kuona washirika wake walioiba fedha au kunufaika nazo, wakifikishwa mahakamani.
7. Amejaribu kuonesha ati kashfa hii walioshughulikia ni CCM, na kwamba kama wangeamua kuiacha isingefika hapa ilipo. Rais anasahau kuwa kashfa hii iliibuliwa na gazeti ka THE CITZEN na mbunge DAVID KAFULILA (NCCR) na kusimamiwa kidete na wabunge wa upinzani, na kwamba wabunge wa CCM walikuwa mbogo baada ya kuona watanzania wamekasirika.
8. Inaonesha kuna mgawanyiko mkubwa sana serikalini, na mambo mengi ambayo Rais kayasema leo yalikywa hayajaamuliwa vizuri, ni kama washauri wake walimuachia yeye mwenyewe amalizie, maana waliona watajikaanga kujaribu kukwepa maazimio ya bunge ambayo yako wazi na yalifikiwa baada ya uchunguzi mkubwa.
9. Kikwete ataondoka madarakani huku 9|10 ya maazimio ya bunge hayajatekelezwa.
10. Viongozi wa CCM, Kinana na wenzake, watakuwa hawajaridhishwa kabisa na maamuzi ya JK, ukizingatia kwamba wamekuwa wakizunguka nchi kusisitiza kuwa watu wote walionufaika na fedha za ESCROW washitakiwe na wanyang'anywe mali zao. Pia rejea kauli za NKM wa CCM, Mwigulu Nchemba, wakati akiwa bungeni.
J. Mtatiro,
Jtatu, 22 Dec 2014,
Dar Es Sa

No comments: