Monday 12 January 2015

KAFULILA ATAKA WALA RUSHWA WAENDE KOROKORONI

Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila amesema kuna kila sababu wahusika wote wa sakata la uchotwaji Sh306 bilioni kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow, wawe wamefukuzwa kazi kabla ya kuanza kwa mkutano ujao wa 18 wa Bunge.Pia, amesema fedha zilizochotwa zirejeshwe kama ilivyokuwa katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) na wafikishwe mahakamani.Akihutubia mamia ya wananchi kwenye Viwanja vya Mwembeyanga jijini Dar es Salaam jana, Kafulila alisema kilichojitokeza katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya ufisadi huo ni ‘trela’ na picha kamili iko katika ripoti ya Takukuru.
“Tunataka kabla ya mkutano kuanza wahusika wote wafukuzwe kazi kwani wamesababisha hasara isiyohitaji mjadala.“Kama ambavyo fedha za Epa zilirejeshwa, na fedha za Escrow nazo zinatakiwa kurejeshwa na zielekezwe katika miradi mingine ya maendeleo kuliko kuwafumbia macho hawa,” alisema Kafulila.Hadi sasa, Rais Jakaya Kikwete ameshamfukuza kazi Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka huku akimweka ‘kiporo’ Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.Wengine waliofikwa na kadhia hiyo ni katibu mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi aliyesimamishwa kupisha uchunguzi, huku aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Fredrick Werema akijiuzulu wadhifa wake kwa maelezo kuwa ushauri wake haukueleweka.Kafulika alisema: “Kuna ripoti ya PCCB ambayo imefichwa na serikali kuhusu sakata hili la escrow na hii tunayoipigia kelele ni trela kwani hiyo ya PCCB ndiyo ina majina na kiasi cha fedha walichokuwa.

No comments: