Thursday 29 October 2015

CCM WANAPENDA NAMBA ILA HAWAJUWI HESABU


uchaguzi huu  wa mwaka 2015 nchini Tanzania umegubikwa na dosari nyingi kwa hio wafaa kurudiliwa pia ni vyema pawe na Tume ya kimataifa huru itakayoshirikisha wote kwenye uchaguzi pasi na kupendelea huyu wala yule.Ufwatao hapa cini ni moja ya  ushahidi wa UKAWA kuonesha kuwa Huyo uchaguzi uligubikwa na Dosari ebu fatilia hapa:


MATOKEO YA NEC YANA KASORO NYINGI.!

1. Tunduma matokeo yametangazwa mara mbili. Jana walisema Lowassa kapata kra 6,000+ leo wametangaza matokeo halisi ya Tunduma kua Lowassa kapata kura 32000+. Matokeo ya jimbo la Tunduma yamerudiwa leo baada ya jana watu kupinga na kuonesha wazi kuwa kulifanyika udanganyifu. Kitendo cha kurudia matokeo mara mbili jimbo moja kinatilia shaka intergrity ya Tume.

2. Jimbo la Bumbuli matokeo ya Ubunge yanaonesha kuwa waliopiga kura ni watu 20,512 ambapo January Makamba amepata kura 17,805.  Lakini cha ajabu kwenye matokeo ya Urais jimbo hilohilo la Bumbuli waliopiga kura ni watu 44,011 ambapo Magufuli anadaiwa kupata kura 35,801.

Sasa jiulize imekuaje waliopiga kura za mbunge wawe watu 20,512 halafu kura za Rais wawe 44,011. Yani kuna watu 24,000 walienda vituoni kupiga kura za Rais tu lakini hawakupiga za Mbunge. Haya ni maajabu ya dunia. Haihitaji degree kujua kwamba Tume imeongeza wapiga kura hewa 24,000 na kura zote hizo wakampa Magufuli.

Niliwahi kusema "CCM wanapenda namba lakini hawajui hesabu". Kiazi kama January ndo anapewa kazi ya kuiba kura za Lowassa unategemea nini? Haiwezekani watu 24,000 waende kituoni kumpigia kura Rais tu halafu wasipige za Mbunge. Utaratibu ulikua watu kupiga kura 3. Sasa iweje waliopiga kura za Urais Bumbuli wawe wengi kuliko waliopiga za Mbunge? Yani mtu alienda kituoni akapewa karatasi ya Rais tu, alipopiga akaondoka bila kupiga ya Mbunge?.

3. Majimbo mengi asilimia za kura zimeonekana kuzidi 100 jambo ambalo linadhihirisha wizi wa waziwazi. Jimbo la Monduli Arusha Lowassa anatajwa kupata kura 49,675 na Magufuli kura 11,335 lakini wote wametajwa kuwa na asilimia zinazolingana (18%).

Jimbo la Arusha Mjini Lowassa anatajwa kupata kura 150,107 na Mgombea wa Chauma amepata kura 551 lakini wote wametajwa kuwa na asilimia zinazolingana (69%). Yani Lowassa amelingana na Hashim Rungwe jimbo la Arusha mjini.

Jimbo la Ndanda ukijumlisha asilimia za wagombea zinakuja 108%. Jimbo la Arusha mjini zinakuja asilimia 182% na majimbo mengine hivyo hivyo. This means waliopewa kazi ya kuiba kura walikosa umakini. CCM wanapenda namba lakini hawajui hesabu.

4. Baadhi ya majimbo idadi ya kura zilizopigwa imezidi idadi ya wapiga kura. Kwa mfano ukijumlisha matokeo ya Jimbo la Makunduchi Zanzibar kwa wagombea wote utapata kura 10,382. Lakini idadi ya kura halali ni 10,352. Yani kura zilikua nyingi kuliko idadi ya wapiga kura. Sasa sijui kama kuna watu walipiga kura mara mbili au vp. CCM wanapenda namba lakini hawajui hesabu.

Hali hiyo pia imejitokeza katika jimbo la Kilindi, jimbo la Bumbuli na majimbo mengine. Hii inapaswa kuingia kwenye kitabu cha records za dunia (Guiness) maana ni maajabu kupata kura nyingi kuzidi idadi ya wapiga kura.

Mwaka 1927 aliyekua Rais wa Liberia Charless King aliingia kwny kitabu cha Guiness baada ya Tume ya uchaguzi nchini humo kumtangaza kuwa ameshinda kwa kura 234,000 wakati idadi ya wapiga kura nchini kwake ilikua 15,000 tu. NEC nao wamefuata nyayo za Charless King. Wanapenda namba lakini hawajui hesabu.

5. Kwa mujibu wa NEC jimbo la Bumbuli na Bukoba mjini ndio majimbo yenye watu smart kuliko majimbo yote Tanzania maana ndio majimbo pekee ambalo hakuna hata kura moja iliyoharibika.

Kwa mfano Bumbuli Idadi ya wapiga kura ni watu 44,011 na idadi ya kura halali ni 44,011. Haya ni maajabu mengine ya dunia. Yani ktk watu 40,000 hakuna hata mmoja aliyekosea. These people are very smart.

Ni ajabu jimbo la Makunduchi Zbar lenye wapiga kura 10,000 walioharibu kura ni watu zaidi ya 100 lakini jimbo la Bumbuli lenye wapiga kura zaidi ya 40,000 hakuna hata mmoja aliyeharibu kura. Kama unaelewa Probability utajua huu ni uongo wa kiwango cha PhD. Watu 44,000 are more likely kuharibu kura nyingi kuliko watu 10,000. KaJanuary hakajui hii formular coz kanapenda namba tu lakini hakajui hesabu. Itz shame.

6. Jimbo la Chwaka na jimbo la Uzini yamelingana kwa kila kitu, kuanzia idadi ya wapiga kura hadi kura za wagombea. This i a very unique coincidence ever happen.

Kwa mujibu wa NEC jimbo la Uzini waliojiandikisha ni watu 11,635, na jimbo la Chwaka waliojiandikisha ni watu 11,635. Jimbo la Uzini waliopiga kura ni 8,777 na jimbo la Chwaka waliopiga kura ni 8,777. Jmbo la Uzini Kura halali ni 8,601, na jmbo la Chwaka kura halali ni 8,601. Zilizoharibika Uzini ni 176 na Chwaka ni 176.

Magufuli jimbo la Uzini kapata kura 6,537 na Chwaka amepta 6,537. Lowasa Uzini kapata 1,864 na Chwaka kpata 1,864.  Haya ni maajabu ya 8 ya dunia.

Hii ndio shida ya kuwapa wainga kama kina January kazi ya kuchakachua. Wanakosa umkini hata kwenye mambo madogo hivi. This is shame.

NINI CHANZO CHA YOTE HAYA?

Sababu inayopelekea fraud hii ya kijinga ktk kutangazwa matokeo inasababishwa na Tume kuacha kutangaza matokeo halisi na kuamua kutangaza matokeo wanayopewa na CCM.

Kuna kikosi kazi cha vijana wa CCM wanaofanya tallying na kuwatumia Tume ya Uchaguzi. Kwa hiyo matokeo yanayotoka majimboni hayaendi moja kwa moja Tume, yanapita kwanza kwa vijana wa CCM wanayachezea ndipo yanaenda Tume. Katika kufanya kazi hiyo wanakosa umakini na kukosea hata vitu vidogo kama niliorodhesha hapo.

Licha ya kubadilisha matokeo ya Urais, mbinu nyingine wanaofanya ni kupunguza kura za Lowassa kwa kuongeza kwenye idadi ya kura zilizoharibika. Katika majimbo mengi Lowassa aliyoongoza hata idadi ya kura zilizoharibika ni nyingi.

Hebu jiulize imekuaje jimbo la Arusha mjini watu zaidi ya 5000 waharibu kura? Watu 5000 ni sawa na wakazi wote wa jimbo la Wawi Zanzibar. So ni sawa na kusema jimbo lote la Wawi wameharibu kura. Impossible.!

Mbinu nyingine ni kupunguza kura za Lowassa na kuwaongezea wagombea wa vyama vidogo. Kwa mfano jimbo la Moshi mjini mgombea wa ADC alipata kuta 11 jimbo zima. Na fomu ya matokeo iliyobandikwa ofisi ya Mkurugenzi inaonesha hivyo. Lakini kwenye matokeo yaliyotangazwa na Tume inaonekana amepata kura 186. Ongezeko la kura 175. Ujinga huu wameufanya ktk majimbo mengi.

WAY FOWARD.

Sisi tumefanya tallying ya majimbo yote ya nchi nzima na tunayo matokeo halisi kama yalivyosainiwa na mawakala wa vyama vyote. Matokeo hayo yanaonesha maoni halisi ya watanzania.

Viongozi wa chama wanakutana leo na muda si mrefu watatoa tamko. Rais wa Tanzania anachaguliwa na Watanzana, ni vizuri kuheshimu maamuzi yao.!

No comments: