Saturday, 10 October 2015

Lowassa aahidi neema kwa wakulima wa zao la kahawa Kilimanjaro

 
Kada mkongwe wa Chama cha Mapinduzi,aliyejiengua hivi karibuni ,Kingunge Ngombalemwiru akisalimia wakati wa mkutano wa kampeni za kumnadi mgombea Urais kupitia Chadema na Vyama vinavyounda Umoja wa katiba ya wananchi UKAWA uliofanyika katika viwanja vya mashujaa mjini Moshi.Picha zote na Dixon Busagaga wa Busagaga's Orijino Blog.
Kada mkongwe wa Chama cha Mapinduzi,aliyejiengua hivi karibuni ,Kingunge Ngombalemwiru akimkaribisha mgombea Urais kupitia Chadema na Vyama vinavyounda Umoja wa katiba ya wananchi UKAWA ,Edward Lowasa kuzungumza na wakazi wa mji wa Moshi katika viwanja vya Mashujaa mjini Moshi.
Mgombea Urais kupitia Chadema chini ya mwavuli wa vyama vinavyounda Umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) ,Edward Lowasa akizungumza na maelfu ya wakazi wa mji wa Moshi na Vitongoji vyake waliofika kumsikiliza katika mkutano uliofanyika viwanja vya Mashujaa mjini hapa.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ,(Chadema) taifa ,Freeman Mbowe akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Mashujaa Mjini Moshi.

Maelefu ya wananchi waliojitokeza katika mkutano wa kampeni wa mgombea Urais kutia Chadema kwa mwavuli wa vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA,wakionesha ishara ya mabadiliko.
Mwenyekiti mwenza wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi,UKAWA,James Mbatia akizungumza katika mkutano wa kampeni wa kumnadi mgombea Urais ,Edward Lowasa uliofanyika katika uwanja wa Mashujaa mjini Moshi.

Mwenyekiti Mwenza wa vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA,James Mbatia akiwa amemnyanyua mkono na kumuombea kura mgombea Ubunge katika jimbo la Moshi mjini ,Jafary Michael
Mgombea Ubunge katika jimbo la Moshi mjini ,Jafary Michael (Chadema) akizungumza na maelefu ya wananchi waliofurika katika uwanja wa Mashujaa mjini Moshi katika mkutan wa kampeni wa kumnadi mgombea Urais kupitia UKAWA,Edward Lowasa.
****************************************************************************************************************************

NA hapa Lowassa afunika nyumbani kwa Dkt Slaa

Sehemu ya wananchi wa Mji wa Karatu, wakionyesha furaha yao baada ya kuiona Chopa inayotumiwa na Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, wakati ikiwasili kwenye Uwanja wa Mkutano, Mjini Karatu, Mkoani Manyara leo Oktoba 9, 2015.
Kikundi cha Ngoma ya Asili kikitoa Burudani katika Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mbowe, Mjini Karatu, Mkoani Manyara leo Oktoba 9, 2015.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akivishwa vazi rasmi la kimila la kabila la wa Iraki, wakati wa Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mbowe, Mjini Karatu, Mkoani Manyara leo Oktoba 9, 2015.

Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akihutubia wananchi katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mbowe, Mjini Karatu, Mkoani Manyara leo Oktoba 9, 2015.


No comments: