Sunday 24 January 2016

Rais Magufuli atunuku kamisheni kwa wahitimu wa chuo cha mafunzo ya kijeshi Monduli


 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Majeshi Nchini Jenerali Davis Mwamunyange wakati alipowasili  katika chuo cha Maafisa wa Kijeshi Monduli Mkoani Arusha kwa ajili ya kuwatunuku Kamisheni Maafisa wapya wa Jeshi kwa cheo cha Luteni Usu, anayetazama katikati ni Mkuu wa Chuo hicho Meja Jenerali Paulo Peter Massao. 
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipungia mkono wananchi wakati akiwasili kwenye viwanja vya Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli kwa ajili ya kuwatunuku Kamisheni Maafisa wapya wa jeshi kwa cheo cha Luteni Usu.
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipigiwa wimbo wa Taifa kabla ya kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi katika viwanja vya Chuo hicho.
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride kabla ya kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia gwaride lililokuwa likipita mbele yake  kutoa heshima.
 Gwaride la Wahitimu likipita kutoa heshima mbele ya mgeni rasmi  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli .

No comments: