Tuesday, 2 February 2016

KABLA HATUJAWAGUSA BAKWATA HEBU TUMSONE KDG HUYU BWANA

Lubuva ni mtu mweledi katika tasnia ya ubabaishaji na upotoshaji. Amejijengea rekodi kuwa ni mtu mwenye ubaya sana na Zanzibar. Aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar aliyeletwa kwa shindikizo la Rais Julius Nyerere kufuatia shindikizo lake (Nyerere) la kwanza kwa Rais Aboud Jumbe kutaka amfukuze kazi Mwanasheria Mkuu wa kwanza wa Zanzibar Huru , Jaji Wolfgang Dourado kwa vile akikosoa sana Muungano.
Hizo porojo za uhuru wa Tume kweli hayo ni maneno yake Lubuva na mara kadhaa huyarejea. Lakini Jee Tume Huru ni suala "subjective" kiasi kwamba kauli ya Lubuva pekee itoshe kutuaminisha kuwa Tume zetu ni huru? Tuna hakika gani kuwa hapewi maelekezo. Na ushahidi wa kimazingira unaotokana na mambo yanavyoendeshwa kwenye Tume yenyewe unatuaminisha vipi : Tume zetu ni huru au ni mabeki wa CCM kuiokoa isifungwe ? Hivi punde Makamo Mwenyekiti wa Tume "Huru" Jaji Mkuu Mstaafu wa JMT , Jaji Augustino Ramadhani aliibukia Dodoma akiwa na kadi yake ya CCM na kugombea kuteuliwa kuwa Mgombea Urais!!!

Suala kama Tume ni huru ni suala objective ambapo vipo vigezo makhsusi vilivyokubaliwa kimataifa kwamba ili Tume iwe huru ni lazim itimize vigezo hivyo. Suali la kujiuliza ni jee Tume zetu zinakidhi vigezo hivyo. Kigezo cha kwanza cha Tume Huru ni kuangalia namna ya uteuzi wa Wajumbe wa Tume yenyewe. Ni Abunuwas na Juha peke yao wataokubaliana na riwaya kuwa Tume ni huru wakati mchakato wa uteuzi wa Wajumbe sio shirikishi na hufanywa na mtu mmoja pekee, tena kwa usiri mkubwa, mtu ambaye ni Mwenyekiti wa Chama chenye wagombea wa kila ngazi Nchi nzima. Mcheza Mechi mmoja peke yake anaamua Referee wa kuchezesha mchezo.
Na vigezo vinginevyo kadhaa vipo. Porojo za Lubuva ni za kujikosha ili yeye aonekane yuko huru. Ni kweli yuko huru lakini ni uhuru wa kuibeba CCM tu.
Kwa kuwaangalia tu na kama unawajua kwa undani , Lubuva na Hamid Mahmoud ni watu huru wa kutenda haki kweli !!!!

No comments: