Monday, 27 May 2013

ZANZIBAR TO DEMAND INDEPENDENCE LISTEN TO CONFERENCE TWO YEARS OF GOVERNMENT OF NATIONAL UNITY IN ZANZIBAR


Democratic and Free Zanzibar will open its embassies over seas and we will built diplomatic areas for All Ambassadors who want to represents there countries here in Zanzibar

<


 • MAPENDEKEZO YA KAMATI YA MARIDHIANO ZANZIBAR KUHUSU UPI UWE MWELEKEO WA WAZANZIBARI KATIKA KUIJADILI RASIMU YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ITAKAYOTOLEWA NA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA
  UTANGULIZI:

  Baada ya wananchi wa Zanzibar kutoa maoni yao juu ya vipi uungano wa Zanzibar na Tanganyika unapaswa kuwa, hatimaye Tume ya Mabadiliko ya Katiba inatarajiwa kutoa rasimu ya awali ya Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kati ya mwishoni mwa mwezi Mei na mwanzoni mwa mwezi Juni 2013.
  Wakati tunaisubiri kwa hamu rasimu hiyo itolewe na kujua kilichomo, sisi wajumbe wa Kamati ya Maridhiano Zanzibar tumekaa na kutafakari juu ya upi unapaswa kuwa mwelekeo wa Wazanzibari katika kuijadili rasimu hiyo pale itakapotoka.
  Baada ya mashauriano ya kina kati ya wajumbe wa Kamati ya Maridhiano na pia kwa kuwahusisha watu wengine mashuhuri hapa Zanzibar, tumekuja na mapendekezo yafuatayo ambayo leo hii tunayawasilisha kwa wananchi wa Zanzibar kupitia Kongamano hili. Haya si maagizo bali ni mashauri yenu na pindi mkiyakubali basi tutakuombeni tuyafanyie kazi kwa pamoja kwa kuyatumia katika kuipokea na kujadili rasimu pale itakapotolewa.
  Mapendekezo yetu ni kama ifuatavyo
  :
  1. Jina la Muungano:
  Muungano huu umetokana na Jamhuri mbili kuungana kwa hiyari. Jamhuri hizo ni Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika. Jina la awali lililotajwa katika Mkataba wa Muungano la muungano wa jamhuri hizi mbili lilikuwa ni Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Jina hili baadaye mwezi Oktoba 1964 lilibadilishwa na kuitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  Ukiangalia mifano ya nchi nyingine zilizoungana, jina la muungano huweka bayana kwamba zilizoungana ni zaidi ya nchi moja, zaidi ya falme moja au zaidi ya jamhuri moja. Kwa mfano, muungano wa nchi (states) za Marekani unaitwa kwa kiingereza United States of America (USA), ule uliokuwa muungano wa jamhuri za kisovieti ukiitwa Union of Soviet Socialist Republics (USSR) na ule muungano wa falme za kiarabu unaitwa United Arab Emirates (UAE).
  Ili kuondosha dhana iliyojengeka kwamba muungano wa jamhuri zetu mbili umeunda nchi moja na kuzifuta nchi zetu, Katiba Mpya inapaswa kuweka jina linalotambua msingi huo na historia hiyo. Hivyo basi, jina jipya liwe ni Muungano wa Jamhuri za Tanzania na kwa kiingereza United Republics of Tanzania.
  Jina hili litasaidia utambulisho wa nchi wanachama katika uwanja wa kimataifa pale litapoambatanishwa katika nyaraka zote rasmi pamoja na jina la nchi husika. Kwa maana hiyo katika uwanja wa kimataifa na katika pasi za kusafiria utaweka wazi na kuwa na

  “UNITED REPUBLICS OF TANZANIA – REPUBLIC OF ZANZIBAR” na “UNITED REPUBLICS OF TANZANIA – REPUBLIC OF TANGANYIKA”.
  2. MIPAKA BAINA YA ZANZIBAR NA TANGANYIKA :
  Wakati zinaungana, Zanzibar na Tanganyika zilikuwa tayari ni nchi zenye mamlaka kamili zikiwa ni wanachama wa Umoja wa Mataifa na hivyo kila moja ilikuwa na mipaka yake inayoeleweka. Katiba na sheria za nchi mbili hizi ziliweka bayana mipaka hiyo na mipaka hiyo ilitambuliwa chini ya sheria za kimataifa.
  Rasimu ya Katiba Mpya ni lazima itamke kwa uwazi kabisa na kutambua na kuheshimu mipaka ya nchi mbili hizi kama ilivyokuwa kabla ya siku ya Muungano tarehe 26 Aprili, 1964.
  Baada ya hapo, Katiba ya Zanzibar na Katiba ya Tanganyika (itakayotungwa baada ya kupata Katiba mpya ya Muungano) kila moja iweke wazi mipaka yake.
  3. URAIA:
  Uraia ndiyo msingi wa ujananchi. Kwa vyovyote vile Katiba Mpya isijumuishe suala la Uraia kuwa la pamoja kupitia Muungano. Kila nchi mwanachama katika muungano ibakie na uraia wake na iratibu masuala yote yanayohusu uraia wake na raia zake. Kwa kufuata mfano kama wa Muungano wa Ulaya (European Union), unaweza kuwa na haki inayotambulika kikatiba ya uhuru wa raia wa nchi moja mwanachama kwenda katika nchi nyengine mwanachama kupitia utaratibu maalum utakaowekwa (free movement of people). Hata hivyo, kila nchi mwanachama iwe na haki ya kuweka utaratibu wa vipi raia hao watafaidi haki na fursa za nchi mwanachama nyingine.
  Hili ni la muhimu hasa kwa nchi ndogo kama Zanzibar ambayo ina rasilimali ndogo ya ardhi na hasa ikizingatiwa kuwa ardhi ilikuwa mojawapo ya sababu kuu za kufanyika Mapinduzi. Katika hali kama hiyo, Zanzibar ina sababu nzito za kuona inadhibiti na kusimamia wenyewe Uraia wake na utambulisho wa raia hao.
  Hivyo basi, suala la Uraia lisiwemo katika mambo ya Muungano na badala yake kila nchi isimamie yenyewe masuala ya Uraia.
  Hata hivyo, kunaweza kukawepo chombo cha pamoja kinachojumuisha nchi mbili hizi cha kuratibu masuala ya Uraia na haki na fursa ambazo raia wanaweza kuwa nazo kwa kila upande.  4. UHAMIAJI :
  Kutokana na sababu tulizozitaja hapo juu kuhusiana na suala la Uraia inapelekea wazi kuwa kila nchi mwanachama idhibiti na kusimamia wenyewe mambo ya Uhamiaji. Hivyo basi, rasimu ya Katiba Mpya isijumuishe suala la Uhamiaji kuwa ni suala la Muungano.
  Kila nchi mwanachama kati ya Zanzibar na Tanganyika iwe na paspoti yake yenyewe yenye kubeba jina la nchi yake na nembo yake ya Taifa na yenye kudhamini usalama wa raia wake nje ya nchi kupitia uhakikisho unaotolewa na Serikali ya nchi husika.
  Ili kuonesha sura ya kuwepo muungano wa kisiasa, paspoti za nchi mbili hizo zinaweza kuwa na jina la Muungano juu na kufuatiwa na jina la nchi mwanachama likiambatana na nembo ya Taifa ya nchi hiyo. Kwa mfano, “UNITED REPUBLICS OF TANZANIA – ZANZIBAR PASSPORT” na “UNITED REPUBLICS OF TANZANIA – TANGANYIKA PASSPORT”.
  Kwa upande mwengine kunaweza kukawa na mamlaka ya kuratibu masuala ya uhamiaji wa nchi hizi mbili (Union immigration regulatory authority) kwa lengo la kuweka na kuratibu mfumo mzuri wa mawasiliano kati ya mamlaka za uhamiaji za nchi mbili hizi.
  5. MAMABO YA NJE :
  Mamlaka juu ya mambo ya nje na uwezo wa nchi kuingia mikataba na nchi nyingine na mashirika ya kimataifa ndiyo roho ya nchi yoyote duniani kutambulika kimataifa na kuweza kusimamia mamlaka yake ya ndani yanapohitaji mashirikiano na nchi nyengine.
  Ili nchi iweze kutambulika kimataifa inapaswa kuwa na mambo manne yafuatayo:
  (a) eneo la ardhi lenye mipaka inayotambulika;
  (b) watu wanaoishi kwenye eneo hilo wanaojitambulisha na eneo hilo;
  (c) serikali inayotekeleza majukumu yake; na
  (d) uwezo wa kuingia katika mahusiano ya kimataifa na nchi nyengine.
  Kwa msingi huo, Wazanzibari wanahitaji kuona kuwa Mambo ya Nje haijumuishwi katika orodha ya mambo ya Muungano na badala yake kila nchi isimamie yenyewe mamlaka yake juu ya mambo ya nje.

  Hata hivyo, uratibu wa sera ya mambo ya nje (foreign policy coordination) inaweza kuwa ni suala la muungano lakini utekelezaji wake kila nchi ikausimamia kupitia Wizara yake ya Mambo ya Nje. Uratibu wa sera ya mambo ya nje unaweza kufanywa kupitia chombo cha pamoja kitakachoundwa na Wizara za Mambo ya Nje za nchi mbili hizi kwa mfano kuwa na Council on Foreign Policy.
  Kutokana na hoja hizo hapo juu inabaki kuwa kila nchi iwe na uanachama na kiti chake katika Umoja wa Mataifa na jumuiya nyengine za kimataifa. Hayo si ajabu katika miungano. Umoja wa Jamhuri za Kisoshalisti za Kisovieti (USSR) ulikuwa na uanachama na kiti chake Umoja wa Mataifa lakini miongoni mwa nchi wanachama, Jamhuri tatu za Ukraine, Belarus na Georgia ziliamua kuwa na uanachama na viti vyao katika Umoja wa Mataifa na hilo liliwezekana.
  Kwa msingi huo huo, Zanzibar iwe na uanchama wake katika Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, Jumuiya ya Madola, Jumuiya ya Afrika Mashariki, Jumuiya ya SADC na jumuiya nyengine za kikanda na za kimataifa.
  6. SARAFU
  , Benki Kuu, Mikopo na Biashara ya Nchi za Nje, Ushuru wa Forodha, Kodi ya Mapato na Kodi ya Mashirika:
  Uchumi si suala la Muungano hata katika Katiba inayotumika sasa. Hata hivyo, nyenzo za kuendeshea na kusimamia uchumi wa nchi kwa maana ya sera za fedha na uchumi (fiscal and monetary policies) zimeendelea kudhibitiwa kupitia Serikali ya Muungano.
  Vyombo vikuu vinavyosimamia sera hizo ambavyo ni Benki Kuu (BOT), Mamlaka ya Kodi Tanzania (TRA) na Wizara ya Fedha ya Serikali ya Muungano vimekuwa vikifanya maamuzi na kuyatekeleza bila ya kuzingatia kuwa kwa maumbile uchumi wa Zanzibar ambao ni uchumi unaotegemea utoaji wa huduma (service oriented economy) hauwezi kuwa sawa na uchumi wa Tanganyika ambao unategemea rasilimali (resource based economy). Sera za fedha na uchumi zikiwemo zile zinazohusu udhibiti wa sarafu na viwango vya kodi, ushuru na riba katika mabenki zimekuwa zikitungwa bila ya kuzingatia msingi huo wa chumi mbili zilizo tofauti na badala yake mara zote zimeegemezwa kwenye kulinda maslahi ya uchumi wa Tanganyika.
  Sarafu ya pamoja imekuwa ikishuka thamani kwa kasi kila uchao kutokana na sababu nyingi lakini miongoni mwake zaidi zinatokana na uendeshaji mbaya wa uchumi wa Tanganyika. Serikali inapochapisha sarafu zaidi ili kudhibiti mfumko wa bei athari zake zinaikumba pia Zanzibar.
  Zanzibar inahitaji kujikomboa kiuchumi ili iweze kutekeleza malengo ya Mapinduzi kwa wananchi wake na hivyo inahitaji kuwa na mamlaka yake kamili katika kusimamia masuala ya sera za fedha

       ITAENDELEA !

   We will not be divided and we will continue to fight for Zanzibar, we want the Warioba constitution commision review to respect the will of the people of Zanzibar.

   ZANZIBAR WANT ITS INDIPENDENCE .

   No comments: