Thursday 2 April 2015

Terrorist Attack Kenya University

At least 15 people have been killed after al-Shabaab gunmen stormed a university in Kenya, opened fire on dormitories and began separating Muslim and Christian students.
Heavy gunfire was reported in the early hours of Thursday morning at the Garissa University College, 120 miles from the Somalian border, when militants attacked the building. There were over 800 students inside at the time and only 280 have been accounted for so far.Kenya's National Police Service said armed militants shot at campus guards to gain entry, triggering a "fierce shootout". The attackers still managed to get inside one of the student dormitories and some remain trapped inside.




Katika style kama ile ya shambulizi la Westgate Mall, wanamgambo wa al-Shabaab wamevamia na kushambulia chuo kikuu cha Garissa kilichopo katika mji wa Garissa. Zaidi ya watu 15 wameuawa, na wengine zaidi ya 53 wamejeruhiwa.

Mkuu wa jeshi la polisi Kenya, Inspector General Joseph Boinnet amesema kuwa magaidi hao walivamia geti kuu la chuo hicho na kuwarushia risasi walinzi alfajiri saa 5.30, wakati wanafunzi wa Kiislam wakienda kwenye swala ya asubuhi.

Polisi waliokuwepo chuoni hapo walikimbilia katika eneo la tukio na kuanza kurushiana risasi na magaidi hao, ambao walifanikiwa kuingia kwenye mabweni ya wanafunzi.

Polisi wa ziada na wanajeshi waliitwa kuja kusaidia na mirindimo ya risasi ilisikika kati ya wavamizi hao, polisi na wanajeshi.

Wanafunzi waliokuwa wakipiga simu kutoka ndani ya mabweni wamesema kuwa kuna majeruhi wengi sana.

Wanafunzi waliofanikiwa kutoroka wamesema kuwa idadi ya wavamizi hao ni angalau watano na bado kuna wanafunzi na maprofesa wengi wanashikiliwa mateka.

Taarifa za hivi punde zinaarifu kuwa magaidi hao wameanza kuwachinja baadhi ya mateka waliowashikilia.

Mateka mmoja (mwanafunzi) mwenye asili ya Somalia aliyeachiwa huru na magaidi hao ameviambia vyombo vya habari vya Kenya kuwa wanafunzi kadhaa wamekwishauawa na miili yao imetapakaa ndani ya vyumba na madarasa huku zoezi la Uchinjaji wa mateka wengine walio hai likianza.
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametuma salamu za rambi rambi kwa familia za wale waliouawa katika shambulizi hilo.
Kenyatta amewataka wakenya kuwa watulivu wakati huu ambapo maafisa wa usalama wanakabiliana na wapiganaji hao.



Wanajeshi wa jeshi la Kenya katika geti la chuo hicho
Baadhi ya miili ya marehemu waliouawa katika shambulio la al-Shabaab katika chuo kikuu cha Garissa



Helicopter ya jeshi ikitua na maiti na baadhi ya majeruhi katika kambi ya jeshi la Langata

Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Excel, iliopo karibu na chuo kikuu cha Garissa wakiondolewa kutoka shuleni kuhakikisha usalama wao

No comments: