Saturday 30 May 2015

Morani wa Kimasai akitisha chama chake


Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid katikati ya Jiji la Arusha umeshuhudia kwa mara nyingine kujaa kwa watu ambao walikuja kwa ajili ya kushuhudia Mbunge huyo akitangaza nia rasmi kabisa kwamba atagombea Urais mwaka huu.May 30 2015 inakuwa siku ambayo inaingia kwenye Historia kubwa kwenye ishu za siasa Tanzania.. Bado miezi michache ufanyike Uchaguzi Mkuu, mmoja ya watu ambao walitajwa sana na kuwa kwenye headlines kubwa kwenye vyombo vya habari ni Mbunge wa Monduli, Edward Ngoyai Lowassa.

Watanzania Wengi walitegemea Lowassa kuzungumzia Rushwa na Mchakato wa Katiba uliofeli. Bali Alitoa speech ya Matumaini na kusema Watanzania wanahitaji mabadiliko, nina uwezo wa kusimamia mabadiliko hayo.. Mwalimu Nyerere alisema Watanzania wasipoyapata mabadiliko hayo ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM.


Aliendelea kwa kusema Nchi yetu inahitaji viongozi wenye sifa hizi.. uongozi wenye uthubutu usioogopa kufanya maamuzi magumu, uongozi usioyumba.. Aweze kuwaunganisha Watanzania na kutoa utofauti kati ya walio nacho na wasio nacho

Kwa wingi wa rasilimali tulizonazo tuna kila sababu ya kutokua  ombaomba… Haya ninayoyaeleza ndio msingi wa utendaji juu ya uongozi wangu utaleta mchakamchaka wa maendieleo ya Serikali nitakayoiongoza nikichaguliwa.. nimeamua kugombea Urais ili kupambana na umaskini.. 


Najua Watanzania wangapi wanaishi kwa bodaboda, mama ntilie.. hawa ni rafiki zangu hawatafukuzwa barabarani.. ni raia wa Tanzania wanaostahili kula kama wewe
Kwenye michezo tumechoka kuwa kichwa cha mwendawazimu, tutaibadili hali hii kwa kasi sana.

No comments: