Monday 18 January 2016

TANZANIA ISHITAKIWE JUMUIA YA MADOLA PIA KWA KUHARIBU DEMOKRASIA ZANZIBAR

KAMATI ya Migogoro na Usuluhishi ya Bunge la Afrika Mashariki (EALA), imepanga kuanza kusikiliza maelezo ya Serikali ya Burundi na chama tawala dhidi ya hoja za wanaharakati wa haki za binadamu na vyama vya kiraia kutaka ifutiwe uanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Vikao hivyo vinatarajiwa kuanza Januari 25 hadi Februari 4, mwaka huu kama njia ya kutafuta ufumbuzi wa kudumu baada ya wanaharakati hao kuwasilisha maombi mbele ya kamati hiyo ya Bunge.
Katika hoja yao, wanaharakati hao wanaliomba Bunge hilo likutane, kujadili na kutoa azimio la mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini humo, baada ya Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza kutangaza kujiongezea muhula wa utawala.
Akizungumza mjini hapa juzi mara baada ya kukamilika kwa hatua ya kusikiliza, kujadili na kuwahoji wanaharakati hao Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Migogoro na Usuluhishi, Dk. Abdullah Mwinyi, alisema tayari wameshafanya mawasiliano na Serikali ya Burundi kwa ajili ya kikao hicho.
Alisema siku ya kwanza walalamikaji ambao ni vyama vya kiraia walipata fursa ya kuwasilisha malalamiko yao ambayo yalisikilizwa.
Mwenyekiti huyo alisema siku ya pili ilifuatia zamu ya wadau ambao ni watu kutoka taasisi na asasi zisizo za kiserikali, walisikilizwa na kuhojiwa.
“Tulipokea barua yao na tukawashukuru kwa kukubali kufika. Lakini tumewaomba wafike Januari 25, mwaka huu kwa ajili ya kuwasikiliza, watasema watakayoyasema na tutawauliza maswali baada ya hapo tutakaa kamati yetu kupitia yote yaliyozungumzwa,” alisema Mwinyi na kuongeza:
“Baada ya hapo tutatayarisha ripoti tutakayoiwasilisha ndani ya Bunge ambako nako itajadiliwa na wabunge kisha kupitisha maazimio yatakayowasilishwa kwenye Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao nao watawasilisha mbele ya wakuu wa nchi wanachama,” alisema.
Alisema dhamira ya kamati yake ni kuhakikisha wanamaliza kusikiliza pande zote wakati wa vikao vya Bunge vinavyotarajiwa kuanza Januari 25, mwaka huu mjini Arusha.

No comments: