Sunday 24 April 2016

Wanaomkosoa Magufuli ni wazalendo wafia nchi Posted by: Mwandishi Wetu 6 hours ago 0 Comments 536 Views Tweet 36 Share 1 Share Pin Mail RAIS John Magufuli ana staili yake ya uongozi – kwa kauli na vitendo – lakini inaaza kumfanya aonekane “dikteta mtarajiwa,” anaandika Ansbert Ngurumo. Baadhi ya wananchi waliokuwa wamekata tamaa, waliochoshwa na uzembe wa utawala uliopita, wanamsifu. Wanadiriki kusema, “bora awe dikteta, lakini tupate maendeleo.” Kwa watu wanaojua udikteta ni nini, hii ni kauli ya kishamba. Sisi tunataka kiongozi mkali, si dikteta. Rais Magufuli ni mkali. Ningependa aendelee kuwa mkali. Atasaidia sana kunyosha yaliyopinda. Atawezesha yaliyoshindikana. Ataweza yaliyowashinda baadhi ya watangulizi wake. Nina uhakika kwamba katika kipindi cha utawala wa Rais Magufuli, kuna mambo atafanikisha kwa sababu ya ukali wake. Lakini sitamani awe dikteta. Na kama tunataka asiwe dikteta, tuanze kumdhibiti sasa. Tumwelekeze. Tumshauri. Hata kama anakataa kushauriwa, tumlazimishe. Tukishindwa kufanya hivyo, akafanya atakavyo, ipo siku tutatamani bora asingezaliwa! Sifa kuu ya madikteta ni kupenda sifa. Wanapenda kuzungumza sana, kuhutubia wengine, kuliko kusikiliza. Wanapenda kusikilizwa, si kukosolewa. Madikteta ni watawala wasiolazimika kufuata katiba, sheria; wanaotawala kwa kutoa matamko, na wasiopenda kusahihishwa. Madikteta si watu wema. Ni watawala katili na wagandamizaji. Kwa sababu hiyo, sitaki Magufuli awe dikteta. Nataka abaki na wema na ukali wake, asiachiwe kuteleza hadi viwango vya udikteta. Natoa onyo hili nikizingatia angalizo la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, aliyesema kuwa kwa katiba ya nchi iliyopo, rais akiamua kuwa dikteta hakuna mtu wa kumzuia. Katiba inampa rais madaraka ya kidikteta. Matumizi yake hutegemea busara zake. Basi. Kwa hiyo, akipatikana rais mwenye “busara ya kuazima” anaweza kulazimisha mfumo wa serikali ambaounakabidhi madaraka yote kwa mtu mmoja (yeye) au kikundi cha watu wachache wanaomzunguika, ambao wakishaamua jambo hakuna mtu wa kuwarudisha nyuma. Waliosoma historia wanajua orodha ndefu wa madikteta. Hata ambao hawakusoma historia wanaweza kujielimisha sasa. Kaisari wa Roma alikuwa dikteta. Mao Zedong wa China alikuwa dikteta. Adolf Hittler wa Ujerumani alikuwa dikteta. Joseph Stalin wa USSR alikuwa dikteta. Josip Broz Tito wa Yugoslavia alikuwa dikteta. Iddi Amin Dada wa Uganda alikuwa dikteta. Mobutu Sese seko wa Zaire alikuwa dikteta. Francisco Franco wa Hispania alikuwa dikteta. Mikono yao iliondoka na damu ya raia wao wasio na hatia, wenye akili nzuri, timamu ya kuhoji na kutaka kusaidia nchi zao zisonge mbele. Wengi wao waliingia madarakani kwa makofi, lakini waliondoka kwa laana. Orodha yao ni ndefu. Sitaki rais wangu awe sehemu ya kundi hili. Sitaki! Hata hivyo, nasikitika kwamba jitihada za serikali ya Rais Magufuli kuzima sauti za wanyonge, ili aseme yeye tu na kupigiwa makofi, zinatia shaka; na zinaweza kumchonga awe dikteta. Kitendo cha serikali yake kufuta gazeti la MAWIO, Januari 17, 2016, si cha kishujaa. Wenzake huko nyuma, wamekuwa wanafungia magazeti. Yeye amefuta. Ameua na kuzika mkondo wa taarifa. Hizi ni tabia za kidikteta. Serikali yake inaonekana kuogopa Bunge. Inapenda wabunge kibogoyo. Tayari inatuhumiwa kuingilia kazi ya Spika katika kupanga kamati za Bunge. Inalenga kunyima wabunge sauti, hasa katika kamati nyeti zinazopaswa kusimamiwa na wapinzani – zinazohusu hesabu za serikali, mashirika ya umma, na serikali za mitaa. Hii ni dalili ya udikteta. Serikali ya Magufuli haitaki wananchi wasikie na kuona moja kwa moja jinsi wabunge wao wanavyojenga hoja kuibana na kuwatetea. Imelazimika kutumia hoja za uwongo kuhalalisha uamuzi wake Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kuzuia matangazo ya Bunge moja kwa moja kama ilivyokuwa. Wakimtumia Nape Nnauye, waziri mwenye dhama ya habari, walisema TBC haitaweza kurusha matangazo hayo kwa sababu ya ukosefu wa fedha. Lakini Tanzania Media Foundation ilijitokeza baadaye na kusema ipo tayari kuwapatia fedha ili watangaze bunge. Hawakufanya jitihada zozote kuzichukua. Sasa wamezuia chombo chochote kuripoti Bunge moja kwa moja hata kama kina uwezo wa kugharamia matangazo hayo. Maana yake ni kwamba walizuia matangazo kwa hofu ya kisiasa, si kwa kukosa fedha. Wanafunga mchirizi mwingine wa taarifa. Wanataka kuishi gizani, ili kutoka huko, waturushie kile wanachotaka tuone. Huu ni woga wa kifisadi usiofanana na taswira anayojenga Rais Magufuli mbele ya umma. Kuna jambo linafichwa. Rais anajua udhaifu wa serikali yake, lakini hataki wananchi waujue. Hii si hulka ya kizalendo. Anajenga msingi wa kuongoza serikali isiyojiamini, inayoogopa nuru, inayoshabikia giza. Anaibua maswali. Sasa tunataka kujua. Anaficha, au anatarajia kuficha uchafu wa nani? Kwa miezi mitano iliyopita, tumeona kwamba Rais Magufuli anapenda kutumia vyombo vya habari kujitangaza, lakini haamini kuwa uhuru wa vyombo vya habari ni nguzo ya demokrasia. Na juzi Jumanne, kwenye uzinduzi wa daraja la Kigamboni, Rais Magufuli aliwaambia waandishi wa habari: “Ndugu zangu waandishi wa habari, muitangaze Tanzania. Muijenge Tanzania. Tusiwe wepesi wa kuandika mabaya ya Tanzania. Sijui kwanini mabaya ndiyo yanapewa front page (ukurasa wa mbele). “Inawezekana nyie waandishi mnaandika vizuri, ila wahariri wenu wanabadilisha. Sijui hawa wahariri wanatoka wapi. Tanzania ni yetu. Wa kuiua ni sisi, wa kuijenga ni sisi.tusipoi-promote Tanzania sisi, ni nani atai-promote? Ni lazima tuwe wazalendo kwa kuitangaza na kuijenga Tanzania kwa ajili yetu na vizazi vijavyo.” Ni kweli kwamba waandishi wanaweza kutangaza Tanzania, lakini hiyo ni kazi ya serikali kupitia vyombo vyake kadhaa, vikiwamo waziri wa mambo ya nje, mabalozi, bodi ya utalii na taasisi nyingine za serikali. Hata bila kuelezwa, vyombo vya habari zinafanya kazi hiyo kwa kuandika na kutangaza habari ambazo moja kwa moja zinanadi mazuri na mabaya yanayotokea Tanzania, kama tunavyopokea yanayotokea kwenye nchi nyingine. Kwa kawaida, vyombo vya habari hutangaza mabaya yanayokera watawala, yanayokomboa wananchi wanyonge. Kama watawala watakuwa waadilifu, hawana sababu ya kuogopa vyombo vya habari, kwa kuwa hakuna baya lao litakaloandikwa. Lakini kauli ya Rais Magufuli inaonesha ana kinyongo na wahariri, na anajaribu kuwasema kupitia kwa waandishi. Kinachosikitisha ni kwamba naye ameingia katika mkumbo wa watangulizi wake walodhani kwamba waandishi na wahariri wao ni makarani wa watawala. Amekosea. Kama kuna watu wametumikia taifa hili kwa uzalendo mkubwa ni wahariri wasiochoka kuibua ufisadi wa watawala. Kama si wahariri, taifa lisingejua ufisadi wa EPA, ingawa serikali ilimalizia sakata hili kwa kusamehe walioiba fedha, na kudai kwamba kuna waliorejesha fedha hizo. Hili halijaisha, hata kama watawala hawataki. Wahariri ndio walifichua ufisadi wa Richmond, ingawa bado haujaandikwa kwa ukamilifu wake. Bila wahariri tusingeijua ufisadi wa Meremeta wala wa fedha za Escrow. Bila kazi nzuri ya wahariri, mawaziri mizigo wasingejiuzulu. Hata kazi anayofanya Rais Magufuli ya “kutumbua majipu” inayompa sifa, isingewezekana kama wahariri wasingejitoa mhanga. Tatizo ni kwamba kazi ya wahariri inatibua ulaji wa watawala. Nasikitika kwamba Rais Magufuli ameanza kutumbukia kwenye mkumbo wa kudhani kuwa “watawala ndiyo nchi,” ambayo hataki ichafuliwe. Je, Rais Magufuli anataka kutuaminisha kuwa naye anajiandaa kuumiza watakaomkosoa? Rais Magufuli anashindwa kujua kuwa wahariri wanaomulika watendaji wabovu wa serikali wanaoiba au wanaotumia madaraka yao vibaya, ndio wanajenga nchi. Ajue kuwa kitendo cha wahariri na waandishi wanafanya kazi ya kujenga uzalendo wa kiwango cha juu. Wahariri wanaokosoa serikali katika mazingira ya ukatili wa viongozi wa serikali na sheria mbaya zilizopo, ni wazalendo kuliko watawala wanaosubiri kusifiwa na kulindwa wanapokosa uadilifu au uaminifu. Wahariri na waandishi hawafanyi kazi ili kupata sifa, bali kunusuru taifa hili ambalo watawala, rafiki zao, na ndugu zao, wameligeuza shamba la bibi kwa muda mrefu. Kauli hii ya Rais Magufuli si ya kishujaa, wala si ya kizalendo. Nashauri Rais Magufuli atafakari kauli ya Rais Thomas Jefferson wa Marakeni, aliyesema: “kama ningeachiwa kuamua iwapo ni vema kuwa na serikali bila magazeti, au kuwa na magazeti bila serikali, nisingesita kuchagua hili la mwisho (magazeti bila serikali). Maana yake ni kwamba kila mtu lazima apate magazeti hayo na awe na uwezo wa kuyasoma.” 36 1 Review Overview User Rating: Be the first one ! Previous: Chadema yamtumbua Magufuli, Prof. Shivji, Prof. Bana Next: Zanzibar ni kupe katika Muungano? ABOUT MWANDISHI WETU ZAFANANA Martin Shigellah, Mkuu wa Mkoa wa Tanga Jiji la Tanga labebesha walimu mzigo wa Mwenge 6 hours ago Dk. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar Zanzibar ni kupe katika Muungano? 6 hours ago Dk. Vicent Mashinji, Katibu mkuu wa Chadema akihutubia kongamano la Chaso, Mkoa wa Dodoma Chadema yamtumbua Magufuli, Prof. Shivji, Prof. Bana 21 hours ago HABARI ZILIZOPITA April 2016 March 2016 February 2016 January 2016 December 2015 November 2015 October 2015 September 2015 August 2015 July 2015 June 2015 May 2015 April 2015 March 2015 February 2015 January 2015 December 2014 November 2014 October 2014 September 2014

John Magufuli, Rais wa Tanzania
RAIS John Magufuli ana staili yake ya uongozi – kwa kauli na vitendo – lakini inaaza kumfanya aonekane “dikteta mtarajiwa,” anaandika Ansbert Ngurumo. Baadhi ya wananchi waliokuwa wamekata tamaa, waliochoshwa na uzembe wa utawala uliopita, wanamsifu. Wanadiriki kusema, “bora awe dikteta, lakini tupate maendeleo.” Kwa watu wanaojua udikteta ni nini, hii ni kauli ya kishamba.
Sisi tunataka kiongozi mkali, si dikteta. Rais Magufuli ni mkali. Ningependa aendelee kuwa mkali. Atasaidia sana kunyosha yaliyopinda. Atawezesha yaliyoshindikana.
Ataweza yaliyowashinda baadhi ya watangulizi wake. Nina uhakika kwamba katika kipindi cha utawala wa Rais Magufuli, kuna mambo atafanikisha kwa sababu ya ukali wake.
Lakini sitamani awe dikteta. Na kama tunataka asiwe dikteta, tuanze kumdhibiti sasa. Tumwelekeze. Tumshauri. Hata kama anakataa kushauriwa, tumlazimishe. Tukishindwa kufanya hivyo, akafanya atakavyo, ipo siku tutatamani bora asingezaliwa!
Sifa kuu ya madikteta ni kupenda sifa. Wanapenda kuzungumza sana, kuhutubia wengine, kuliko kusikiliza. Wanapenda kusikilizwa, si kukosolewa.

Madikteta ni watawala wasiolazimika kufuata katiba, sheria; wanaotawala kwa kutoa matamko, na wasiopenda kusahihishwa. Madikteta si watu wema. Ni watawala katili na wagandamizaji. Kwa sababu hiyo, sitaki Magufuli awe dikteta. Nataka abaki na wema na ukali wake, asiachiwe kuteleza hadi viwango vya udikteta.
Natoa onyo hili nikizingatia angalizo la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, aliyesema kuwa kwa katiba ya nchi iliyopo, rais akiamua kuwa dikteta hakuna mtu wa kumzuia. Katiba inampa rais madaraka ya kidikteta. Matumizi yake hutegemea busara zake. Basi.
Kwa hiyo, akipatikana rais mwenye “busara ya kuazima” anaweza kulazimisha mfumo wa serikali ambaounakabidhi madaraka yote kwa mtu mmoja (yeye) au kikundi cha watu wachache wanaomzunguika, ambao wakishaamua jambo hakuna mtu wa kuwarudisha nyuma.
Waliosoma historia wanajua orodha ndefu wa madikteta. Hata ambao hawakusoma historia wanaweza kujielimisha sasa. Kaisari wa Roma alikuwa dikteta. Mao Zedong wa China alikuwa dikteta. Adolf Hittler wa Ujerumani alikuwa dikteta.
Joseph Stalin wa USSR alikuwa dikteta. Josip Broz Tito wa Yugoslavia alikuwa dikteta. Iddi Amin Dada wa Uganda alikuwa dikteta. Mobutu Sese seko wa Zaire alikuwa dikteta. Francisco Franco wa Hispania alikuwa dikteta.
Mikono yao iliondoka na damu ya raia wao wasio na hatia, wenye akili nzuri, timamu ya kuhoji na kutaka kusaidia nchi zao zisonge mbele.
Wengi wao waliingia madarakani kwa makofi, lakini waliondoka kwa laana. Orodha yao ni ndefu. Sitaki rais wangu awe sehemu ya kundi hili. Sitaki!
Hata hivyo, nasikitika kwamba jitihada za serikali ya Rais Magufuli kuzima sauti za wanyonge, ili aseme yeye tu na kupigiwa makofi, zinatia shaka; na zinaweza kumchonga awe dikteta.
Kitendo cha serikali yake kufuta gazeti la MAWIO, Januari 17, 2016, si cha kishujaa. Wenzake huko nyuma, wamekuwa wanafungia magazeti. Yeye amefuta. Ameua na kuzika mkondo wa taarifa. Hizi ni tabia za kidikteta.
Serikali yake inaonekana kuogopa Bunge. Inapenda wabunge kibogoyo. Tayari inatuhumiwa kuingilia kazi ya Spika katika kupanga kamati za Bunge. Inalenga kunyima wabunge sauti, hasa katika kamati nyeti zinazopaswa kusimamiwa na wapinzani – zinazohusu hesabu za serikali, mashirika ya umma, na serikali za mitaa. Hii ni dalili ya udikteta.
Serikali ya Magufuli haitaki wananchi wasikie na kuona moja kwa moja jinsi wabunge wao wanavyojenga hoja kuibana na kuwatetea. Imelazimika kutumia hoja za uwongo kuhalalisha uamuzi wake Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kuzuia matangazo ya Bunge moja kwa moja kama ilivyokuwa.
Wakimtumia Nape Nnauye, waziri mwenye dhama ya habari, walisema TBC haitaweza kurusha matangazo hayo kwa sababu ya ukosefu wa fedha. Lakini Tanzania Media Foundation ilijitokeza baadaye na kusema ipo tayari kuwapatia fedha ili watangaze bunge.
Hawakufanya jitihada zozote kuzichukua. Sasa wamezuia chombo chochote kuripoti Bunge moja kwa moja hata kama kina uwezo wa kugharamia matangazo hayo. Maana yake ni kwamba walizuia matangazo kwa hofu ya kisiasa, si kwa kukosa fedha.
Wanafunga mchirizi mwingine wa taarifa. Wanataka kuishi gizani, ili kutoka huko, waturushie kile wanachotaka tuone. Huu ni woga wa kifisadi usiofanana na taswira anayojenga Rais Magufuli mbele ya umma.
Kuna jambo linafichwa. Rais anajua udhaifu wa serikali yake, lakini hataki wananchi waujue. Hii si hulka ya kizalendo.
Anajenga msingi wa kuongoza serikali isiyojiamini, inayoogopa nuru, inayoshabikia giza. Anaibua maswali. Sasa tunataka kujua. Anaficha, au anatarajia kuficha uchafu wa nani?
Kwa miezi mitano iliyopita, tumeona kwamba Rais Magufuli anapenda kutumia vyombo vya habari kujitangaza, lakini haamini kuwa uhuru wa vyombo vya habari ni nguzo ya demokrasia.
Na juzi Jumanne, kwenye uzinduzi wa daraja la Kigamboni, Rais Magufuli aliwaambia waandishi wa habari:
“Ndugu zangu waandishi wa habari, muitangaze Tanzania. Muijenge Tanzania. Tusiwe wepesi wa kuandika mabaya ya Tanzania. Sijui kwanini mabaya ndiyo yanapewa front page (ukurasa wa mbele).
“Inawezekana nyie waandishi mnaandika vizuri, ila wahariri wenu wanabadilisha. Sijui hawa wahariri wanatoka wapi. Tanzania ni yetu. Wa kuiua ni sisi, wa kuijenga ni sisi.tusipoi-promote Tanzania sisi, ni nani atai-promote? Ni lazima tuwe wazalendo kwa kuitangaza na kuijenga Tanzania kwa ajili yetu na vizazi vijavyo.”
Ni kweli kwamba waandishi wanaweza kutangaza Tanzania, lakini hiyo ni kazi ya serikali kupitia vyombo vyake kadhaa, vikiwamo waziri wa mambo ya nje, mabalozi, bodi ya utalii na taasisi nyingine za serikali.
Hata bila kuelezwa, vyombo vya habari zinafanya kazi hiyo kwa kuandika na kutangaza habari ambazo moja kwa moja zinanadi mazuri na mabaya yanayotokea Tanzania, kama tunavyopokea yanayotokea kwenye nchi nyingine.
Kwa kawaida, vyombo vya habari hutangaza mabaya yanayokera watawala, yanayokomboa wananchi wanyonge.
Kama watawala watakuwa waadilifu, hawana sababu ya kuogopa vyombo vya habari, kwa kuwa hakuna baya lao litakaloandikwa.
Lakini kauli ya Rais Magufuli inaonesha ana kinyongo na wahariri, na anajaribu kuwasema kupitia kwa waandishi. Kinachosikitisha ni kwamba naye ameingia katika mkumbo wa watangulizi wake walodhani kwamba waandishi na wahariri wao ni makarani wa watawala. Amekosea.
Kama kuna watu wametumikia taifa hili kwa uzalendo mkubwa ni wahariri wasiochoka kuibua ufisadi wa watawala. Kama si wahariri, taifa lisingejua ufisadi wa EPA, ingawa serikali ilimalizia sakata hili kwa kusamehe walioiba fedha, na kudai kwamba kuna waliorejesha fedha hizo. Hili halijaisha, hata kama watawala hawataki.
Wahariri ndio walifichua ufisadi wa Richmond, ingawa bado haujaandikwa kwa ukamilifu wake. Bila wahariri tusingeijua ufisadi wa Meremeta wala wa fedha za Escrow.
Bila kazi nzuri ya wahariri, mawaziri mizigo wasingejiuzulu. Hata kazi anayofanya Rais Magufuli ya “kutumbua majipu” inayompa sifa, isingewezekana kama wahariri wasingejitoa mhanga.
Tatizo ni kwamba kazi ya wahariri inatibua ulaji wa watawala. Nasikitika kwamba Rais Magufuli ameanza kutumbukia kwenye mkumbo wa kudhani kuwa “watawala ndiyo nchi,” ambayo hataki ichafuliwe.
Je, Rais Magufuli anataka kutuaminisha kuwa naye anajiandaa kuumiza watakaomkosoa?
Rais Magufuli anashindwa kujua kuwa wahariri wanaomulika watendaji wabovu wa serikali wanaoiba au wanaotumia madaraka yao vibaya, ndio wanajenga nchi.
Ajue kuwa kitendo cha wahariri na waandishi wanafanya kazi ya kujenga uzalendo wa kiwango cha juu. Wahariri wanaokosoa serikali katika mazingira ya ukatili wa viongozi wa serikali na sheria mbaya zilizopo, ni wazalendo kuliko watawala wanaosubiri kusifiwa na kulindwa wanapokosa uadilifu au uaminifu.
Wahariri na waandishi hawafanyi kazi ili kupata sifa, bali kunusuru taifa hili ambalo watawala, rafiki zao, na ndugu zao, wameligeuza shamba la bibi kwa muda mrefu. Kauli hii ya Rais Magufuli si ya kishujaa, wala si ya kizalendo.
Nashauri Rais Magufuli atafakari kauli ya Rais Thomas Jefferson wa Marakeni, aliyesema: “kama ningeachiwa kuamua iwapo ni vema kuwa na serikali bila magazeti, au kuwa na magazeti bila serikali, nisingesita kuchagua hili la mwisho (magazeti bila serikali). Maana yake ni kwamba kila mtu lazima apate magazeti hayo na awe na uwezo wa kuyasoma.

No comments: