Sunday, 24 February 2013

Makamu wa Kwanza wa Rais alipotembela Ofisi ya Utambulisho wa MZanzibari au ZANZIBAR ID CARD imeonesha Wazanzibari wengi hata wamepata uvivu kuvichukua vitambulisho hivi kwa vile havitumiki kwa manufaa ya nchi bali vinatumika kisiasa tu . Hivi Karibuni Mkurugenzi wa Vitambulisho alwiwaonesha maboksi ya VItambulisho waandishi wa habari kuwa Wananchi wengine hata hawafuatilii VItambulisho vyao kwa kuchoka na siasa ila imefika Wazanziabri kudai haki zao kuonesha Matumizi ya mamilioni yaliotumika kutengeneza VItambulisho Hivi ni wakati muafaka kuanza kutumika VItambulisho hivi Kabla ya kuanza Intergartion ya Afrika Mashariki miaka michache ijayo kuanza kuwazoesha Wananchi. Nishauri serikali ya GNU Iweke usalma wa Wazanzibari kwanza Iweke uzalendo na siasa baadae Iweke Camera kwenye Majengo yote Makubwa ya Ibada ya DIni zote .Hii Ndio ilivyokua Marekani baada ya Tukio la September 11 Misikiti ya Waislamu ilikua ikishambuliwa na serkali kwa kushirikiana na FBI Waliweka ulinzi kwenye sehemu za Ibada kwenye sehemu inazoingia waumini wengi ili ikitokezea majitu katili kushambulia sehemu hizi wakamatwe. Pia Ningewaomba Viongozi wa Juu wa GNU kurudisha tena ile Sheria ya Wazanzibari wakienda Tanganyika Waoneshe Kitambulisho na wageni Wengine wote Watakaoingia Zanzibar na Wazanzibari wawe na Kitambulisho au Passport, Kuna uwezekano mkubwa Magaidi kuingia na Kushambulia bila ya kuwa na Ulinzi wa kutosha na kujua nani anaingia na kutoka Zanzibar Kuna umuhimu wa kujua faida za Zanzibar ID sio kwa kujiandikisha kupiga kura tu Tupunguze kuifanya Zanzibar ID ni tool ya kisiasa tu . Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amesema kuwa watu wenye nia mbaya wameamua kuyatumia matukio ya kuuawa na kujeruhiwa kwa viongozi wa kidini ili kuvunja umoja wa Wazanzibari .Makamu wa Kwanza wa Rais alisema kinachoonekana kuna ajenda imetayarishwa ya kutaka kulazimisha chuki za kidini Zanzibar, licha ya kuwa Zanzibar ina historia ya miaka mingi ya watu kuvumiliana na kuishi kwa pamoja, pamoja na kuwepo watu wa imani tafauti..Maalim Seif alisema vitendo vya kuuawa na kujeruhiwa viongozi wa kidini Zanzibar ni mambo mageni na kwa miaka mingi Zanzibar imekuwa ni mfano bora wa uvumilivu wa kiitikadi za kidini, licha ya kuwa asilimia 98 ya wananchi wake ni Waislamu.Na pia kulaani tukio la hujuma hizi kuzihusisha na ugaidi .Nasema Zanzibar hakuna ugaidi, hakuna ugomvi wa kidini. Yanayotokea yametusikitisha sana, ni matokeo ya uhalifu wa kupindukia, linaloweza kufanywa lifanywe kuwanasa wahalifu hawa na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sharia,” alisema Makamu wa Kwanza wa Rais. Aliwataka wananchi wote wa Zanzibar kwa wakati huu kuwa watulivu na wasitawaliwe na jazba na wala wasichokozane, pia wasikubali kuchokozeka kitu ambacho DIRAYETU inakiona ni umakini wa Waziri anesimamia Wizara ya Mambo ya Ndani ambae wengi wanamini elimu yake haijulikani hata chuo alichosoma kuna wengine Wanahisi ni Waziri kihiyo.Ila Waziri huyu ameonesha sura yake ya ubaguzi kwa Wazanzibari Kwani tumeona Nyaraka zilizotolewa na Wizara mambo ya ndani juu ya uchunguzi wa Kifo cha MArehemu Mushi kiliweza kufikisha kwenye mwisho wa dunia na kwuahukumu Wazanzibari hata uchunguzi haujafanyika na kuna Website nyengine za Ulaya na Marekani tayari ziliihukumu Jumuia ya Kiislamu ya Uamsho ukitembeela website ya council of Christian imeweka bayana kua ni Uamsho ndio iliomuuwa Mheshimiwa Mushi , Pia tumeambiwa kuwa Rais kikwete ameziomba taasisis za nje kusaidia uchunguzi wa Mauaji ya Mushi ila jana tu tumeona Sheikh mmoja huko Zanzibar ameuliwa kwa kupigwa mapanga , wengi wamewahusisha watu wa dini nyengine kua wameenda Zanzibar kulipa Kisasi ch Mauaji ya Mushi.Hata wengine sasa watu Vijijini huko Zanzibar wamepata woga kuingiliwa na watu wasio vitakia amani Visiwa hivi na kuwaua . Naishauri Serikali ya Zanzibar irudishe tena sheria iliokuwapo huko Nyuma kuwa kila anaeingia Visiwani humo Lazima ajulikane anaenda kufanya nini na Lazima aingie na ID Kitambulisho Kunaweza kungiliwa na magaidi na kuripua mahoteli kama kina ALshabab kwa kupitia Tanganyika kwa vile hakuna kizuizi yakitokeze matukio ya kigaidi Zanzibar kama yale yalioripua Balozi za Mareakani Mwaka 1998 maana yake Utalii ndio umekufa mamai ya watu watakiosa ajira kwa kushindwa kueka usalama , ikiwa hakuna usalama Kwa raia Hata Mgeni hatoweza kuja Zanzibar kwa kuhofia maisha yake .Usalama ni moja ya mambo yanayoimarisha utalii tumeona Egypt Usalama uliposhuka Utalii umeshuka kwua ZERO. Kilichoniumiza Kichwa Zaidi ni vipi Mauaji haya serikali ilivyoonesha Udini na Ubaguzi wa hal ia yajuu kwa Wazanzibari .Rais Mkapa alikwenda kwenye mazishi ya mchungaji wa kanisa la Pentekoste Assemblies of God Mathayo Kachila (45) aliyepoteza maisha kwa kuchinjwa na watu wanaodaiwa ni waumini wadini ya kiislam kisha mwili wake kutelekezwa kwenye vibanda vya maduka na DR Shein na Viongozi wengine wa juu wa Zanzibar. Kushiriki Mazsihi ya Padri Mushi, ambaye ni paroko wa parokia ya Minara Miwili - Zanzibar . Pia jana Watu wasiojulikana wlaimvizia Sheikh au Imamu wa Msiskiti Mmoja huko Zanzibar alipoenda shambani kwake huko Kisiwani Unguja nje ya mji na kumpiga mapanga na kuvuja damu nyingi hadi kufa Hatukusikia media za Tanganyika Kulaani tukio hili kama lile la Paoko Mushi pia hatukuona Mazishi yaliopewa Uzito na Wanasiasa kama yale ya Viongozi wawili wa wlaioluwa mwanzo mabao sio Waislamu. Pia imefikia hata VIongzi wengine wa Upinzani kundika kwenye sicial media zoa kua ni majamabazi ndio waliomuuwa Imam huyu wa Zanzibar La kujiuliza kwani nin iwasiandike kuwa na Huyu Parko Mushi ameuliwa na majamabazi kama Zanzibar imeshindwa kuwe na Usalama au ndio double standard ya udini na ubaguziwa wazi.Pia tuliona Saidi Mwema alivyofika Zanzibar haraka na kutoa Malekezo yake kwa jamii ila hatujaona amelekezo yake kwa Imamu alieuliwa ! Ila Kubwa Zaidi lilionishangaza ni Kwanini Hadi leo hii Vyama vya Upinzani huko Tanganyika na Zanzibar vimeshindwa kushinikiza Waziri huyu awajibike kwani hata kulipokua na Mfumo wa Chama Kimoja Mzee Ruksa alijiuzulu kutokana na watu kumuona alishindwa kutekeleza majukumu yake na Mzee Ruksa alijiuzulu Uwaziri wa Mambo ya ndani na baadae kuweza tena kurudi kwenye siasa ila aliilinda heshima ya Chama chake kwa wakati huo na Watanzania Kumsamehe hadi kufikia kumpa URAIS kwa vipindi viwili. Nikiingia kwenye vipi serikali ilivyo weza ku handle suala hili na uchambuzi wangu juu ya mauaji ya Mapadri hawa wawili Mmoja ameuliwa na Watu waliojulikana kwa tukio la Kuchinja Nyama liliwahusisha Waislamu na Wakristo wa Tanganyika .Na kufikia Waziri Mkuu kufanya kikao cha Viongozi wa Dini kule Mwanza Viongzi wa dini hizi kuu huko Tanganyika walitoa maoni yao nani achinje nyama na mwisho wake Serikali ilisema Waislamu waendelee Kuchinja Nyama. KWa hili Nampongeza Mheshimiwa Mizengio Pinda kwa kuonesha Uongozi KWani kiongozi wa kweli pale panapotokea tatizo ndio huonesha ungozi wake Mtoto wa Mkulima ameonesha ushupavu wa kuwaweka watu pamoja haraka na kutuliza msuguano wa Udini Hapa Nampa A Plus Kiongozi shupavu ni yule anasiamam haraka kbla ya damu kuzidi kumwagika ila Bado Nawashauri Wana CCM kwa heshima yao Waziri Nchimbi hafai kwa Tanganyika na Hasa KWa Wazanzibari ameonesha dharau yake kusema Zanzibar kuna ugaidi wka vile Wazanzibaari asimia 98 ni Waislamu ni ubaguzi usilovumilika Kwa Mzanzibari yoyote Mwenye Chama na asie Chama Ubaguzi huu Lazima ukomeshwe Na Wazanzibari warudushe tena ile Style Mzee Karume Kuwa sheria zao nambo yao mengine Mwisho Kisiwa Cha Chumbe ! Wazanzibari Wamlaani Waziri Huyu Mchimbi Kwa kuwaita Wazanzibari Magaidi. America condems killing of Tanzania Roman Catholic Leader The United States of America strongly condemns the senseless murder of Father Evaristus Mushi in Zanzibar on February 17. We offer sincere condolences to his family, parishioners, and friends. This vicious and cowardly act is the third directed against a religious leader in Zanzibar since November 2012 and goes against the long held values and culture of peace in Zanzibar, a land known for its cultural richness, tolerance, and diversity, where many peoples and cultures have lived and worked side by side for centuries. Religious based violence is crime that has no place in Tanzania or anywhere else. In fact, it goes against the very character that Tanzania has been known for since its founding and the three national pillars carefully nurtured by Mwalimu Julius Nyerere, which are also forever enshrined in the national anthem of this land: Hekima, Umoja, na Amani - Wisdom, Unity, and Peace. The people of Zanzibar and all Tanzanians should reject the violent hatred spread by a very few individuals whose actions threaten to tarnish the peace, security, and image of this wonderful land. The United States stands as a committed partner to all citizens of this land and we urge them to continue to denounce violence committed by those who threaten and undermine the security of their fellow citizens. We also stand ready to assist the Tanzanian justice system as needed, and call for the arrest, prosecution and conviction of those responsible for these heinous crimes against religious leaders in Zanzibar. Finally, we call on all citizens to build on the values of tolerance, wisdom, unity, and peace that are so cherished by all Tanzanians and civilized people of the world. Press statement by U.S. Ambassador Alfonso E. Lenhardt in Tanzania Source: http://www.wavuti.com/4/post/2013/02/zanzibar-padrefather-mushi-emepigwa-risasi-na-kuuawa.html#ixzz2LsFk8kzF 1 .Padri Mushi, ambaye ni paroko wa parokia ya Minara Miwili - Zanzibar amepigwa risasi na watu wasiojulikana mida ya saa moja asubuhi akielekea kanisani kuongoza ibada Padre Mushi aliuawa na watu walipolisimamisha gari la Padre huyo alipokuwa akielekea katika kanisa la Mtakatifu Theresia lililoko eneo la Mtoni, na alipopunguza mwendo ili awasikilize, ndipo alipopigwa risasi kichwani na kusababisha gari alilokuwamo kukosa uelekeo na kuigonga nyumba iliyokuwa jirani. Watu walioshuhudia tukio hilo walimchukua Padre Mushi ili kumwahisha hospitalini katika jitihada za kuokoa uhai wake, lakini alifariki dunia. Waliomwua Padre Mushi bado hawajakamatwa.Watu watatu wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za mauaji ya Padre Mushi. < 2. Pia Machafuko makubwa yametokea katika kijiji cha Buseresere Wilayani Chato Mkoani Geita kati ya waslam na wakristo na kupelekea watu 10 kujeruhiwa vibaya kwa mapanga huku mchungaji wa kanisa la Pentekoste Assemblies of God Mathayo Kachila (45) akipoteza maisha kwa kuchinjwa na watu wanaodaiwa ni waumini wadini ya kiislam kisha mwili wake kutelekezwa kwenye vibanda vya maduka ambavyo vilikuwa jirani na eneo hilo Mkuu wa Wilaya ya Chato Ludorick Mpogolo aliyefika eneo la tukio muda mfupi baada ya polisi kuwasili eneo hilo mbali na kusikitishwa na kitendo hicho aliwataka wananchi kuwa watulivu wakati serikali ikiangalia njia sahihi za kutatua mgogoro huo ambao unakuwa kwa kasi kila kukicha. 3 IMAMU WA MSIKITI WA MWAKAJE ZANZIBAR AULIWA KWA KUPIGWA MAPANGA. Pia Naitaka serikali na Wizara ya mambo ya Ndani iziweke kesi hizi mbili za Zanzibar kwenye Kapu moja kuwa wote wameulwia na Maharamia, Mzanzibari wa Kawaida haruhusiwi Kumiliki Silaha na serikali inajua hao Wafanya Bishara wachache waliopew SIlaha kwa kujilinda Silaha nyingi Zanzibar ziko mikononi kwa Polisi na JWTZ

No comments: