Monday 30 March 2015

Wabunge Wazozana juu ya Mahkama ya Kadhi Bungeni.


Vurugu, matusi na lugha za kejeli ni miongoni mwa mambo yaliyotawala katika semina ya wabunge kuhusiana muswada wa sheria ya kutambuliwa na Serikali, maamuzi yatakayokuwa yakitolewa na Mahakama za Kadhi hapa nchini.

Wabunge walishindwa kuvumiliana na kuheshimiana walipokuwa wakichangia mara baada ya Jaji Robert Makaramba kuwasilisha mada kuhusiana na muswada huo, hali iliyolazimu ulinzi kuimarishwa ndani ya ukumbi huo kwa hofu kwamba huenda waheshimiwa Wabunge hao wangetwangana ngumi.

Ulifika muda ambapo mtu alimtafuta mbaya wake ama kutamka anachokiamini huku lugha za kutishana zikitawala.

Wakihitimisha semina hiyo, Jaji Robert Makaramba na Waziri mkuu Mizengo Pinda walisema ujumbe umefika na mapungufu yaliyoonekana yatafanyiwa kazi.

No comments: