Madaktari kutoka Washington Diaspora Walioletwa na Jumuiya ya Watanzania Washington Wakataliwakutoa Huduma ya Afya Hospitali ya Mnazi Mmoja huko Zanzibar wamenyimwa kibali cha kutoa huduma kwa wananchi.
Dr Nawfal akizungumza na Ujumbe wa Madaktari kutoka Washington Diaspora walipofika katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kutoa huduma ya Maradhi ya Saratani ya Matiti, Kisukari na Tiba ya Meno ukiwa na Ujumbe wa Watu 17, Wamefika Ofisi hapo kujitambulisha kwa Uongozi wa hospitali
Dr Nawfal akizungumza na Madaktari hao walipofika Ofisini kujitambulisha wakiwa na wenyeji wao Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Diaspora Zanzibar Ukiongozwa na Mkurugezi wa Idara hiyo Ndg Adila
Ujumbe wa Madaktari Madiaspora wakimsikiliza Dr Nawfali walipofika Ofisini kwakwe kujitambulisha na kwa ajili ya kutoa huduma kwa Wagonjwa waliofika hospitalini hapo kupata tiba.
Kiongozi wa Jumuiya ya Watanzania Washington Diaspora Asha Nyanganyi akiztowa maelezo ya Ujumbe huo kwa Dr Nawfal wakati walipofika Ofisini kwake Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja leo asubuhi kwa kutoa huduma za Meno, Kisukari kutoa dawa kwa wagonjwa na kutowa elimu ya Saratani ya Matiti kwa Wanawake Zanzibar
No comments:
Post a Comment